Showing posts with label burudani. Show all posts
Showing posts with label burudani. Show all posts

YOUNG DEE AKANUSHA SKENDO YA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

Msanii Young Dee amekanusha uvumi ulioenea mitaani kuwa anajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na kusema kuwa pamoja na story hizo kuwa kubwa lakini hali hiyo haijamuathiri sana kwasababu hazina ukweli wowote.

“Ni story ambazo zimekuwa kubwa sana lakini hazijaniathiri sana kwasababu sio ukweli, lakini zimenifanya nimezidi kuwa makini sana kuwa muoga pia na vitu vingi sana kuangalia watu wanaonizunguka, mazingira na vitu kama hivyo”.
Alisema Young Dar es salaam kupitia E-News ya EATV jana . 
Dee amesema kuwa anafahamu fika kuwa utumiaji wa ‘unga’ unaweza kuathiri kazi yake ya muziki kutokana na mifano hai ambayo imeshaonekana kwa wasanii wengine, 
“The more the story zinakuwa kubwa zinapoteza maana nzima ya kitu nachohangaikia kila siku ambayo ni muziki, so naonekana muziki nafanya nakula unga na mifano ipo watu ambao wameingia kitika hayo mambo”.

Young Dee alimaliza kwa kusema kama kweli maneno yanayosemwa mtaani yana ukweli basi watu watagundua haraka, “mi ambacho naweza kusema unga hauna siri haufichiki so kama mi nakula unga people they can easily notice haraka sana”

NILIINGIA KWENYE MUZIKI KWA KUFUATA MKUMBO: SALMA JABU NISHA

Actress maarufu nchini Salma Jabu(Nisha) amesema kuwa aliingia katika muziki wa Bongofleva kwa kufuata mkumbo baada ya kuwaona waigizaji wenzake wengi wakiingia katika muziki na yeye ndiyo akajitumbukiza na matakeo yake kukaa sana kimya na kupotea katika fani hiyo. Nisha amesema kuwa hatathubutu tena kufuata mkumbo kwenye fani nyingine bali yeye ameamua kujikita zaidi
kwenye fani yake ya filamu. Akizungumza na Gpl star huyo wa filamu za Red-Cross, Matilda, Pusi Na Paku na Tikisa alisema "Niliona waigizaji wanaingia kuimba na mimi nikaingia, nilivamia fani tu ndiyo maana  najuta, nimeamua nikae chonjo kwanza na mambo hayo nijikite zangu kwenye filamu"

WEMA"NINYI MNAZANI NAMWAZA DIAMOND KILA SAA, NO MIMI NAWAZA JINSI YA KU MAKE MORE MONEY""

Wema Sepetu mwenyewe anajua kwamba watu wengi wanafikiri yeye anawaza kuwa na Diamond hivi sasa, lakini ametoa majibu ya hayo mawazo kwenye hii picha. Maana ya hii picha ni kwamba watu wengi wanafikiri kwamba muda wote Diamond yupo kwenye kichwa cha Wema, lakini yeye mwenyewe anasema kwamba muda wote anafikiria pesa. Unaionaje hiyo picha?

LULU AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KUHUSU KESI YA KINA PAPII KOCHA, SOMA HAPA ALICHOKISEMA

Ninaamini Mungu yupo...anasikia,anaona na ndiye mwenye kuhukumu kwa Haki...!!!!Dua zangu ziko pamoja na Mzee Nguza na Papii Kocha...!hakuna linaloshindikana mbele ya Mwenyezi Mungu...Kama anaweza kutoa Jaribu basi yeye pia ndo mwenye Uwezo wa kufanya Njia ya kutoka ktk jaribu Hilo...!Mwenyezi Mungu awasimamie katika rufaa yenu...!AMEN”

Hayo ni maneno ya mwanadada Elizabeth Michael (LULU) aliyoyaandika kupitia kwenye mtandao akiwaombea kheri Mzee Nguza na mwanawe Papii Kocha wanaosubiria kusikilizwa kwa rufaa yao ya kesi ya ulawiti inayowakabili


Toka atoke jela, mwanadada lulu ameonekana kubadilika sana kitabia tofauti na alivyokuwa akionekana hapo awali.

MAKALIO YA KAJALA NI DILI,,MPEMBA AHADI KUUZA NYUMBA ILI AMLE ULODA MSANII HUYO!!

KATIKA hali ya kushangaza, staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amenaswa akiwa ametinga khanga moja na kuwaacha watu midomo wazi.
Kajala alinaswa na kamera yetu maeneo ya Kigogo jijini Dar ambapo watu kibao walionekana kumzunguka na kuhoji kulikoni staa huyo ambaye amezoeleka kutika pamba kali, aonekane na vazi la khanga iliyosababisha makalio yake yaonekana sawia na kuwavutia wanaume wakware?
Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Kajala alisema alilazimika kutinga khanga hiyo kuendana na matakwa ya filamu yaliyomtaka kuvaa vazi hilo na kuonesha mazingira ya uswahilini hivyo watu waliomzunguka walikuwa hawajui nini kinaendelea.
Nilipoambia naigiza sinema ya Kigodoro nilishtuka sana lakini mwisho wa siku nilikubali kwa kuwa mimi ni msanii naweza kubadilika kivyovyote na nina imani mashabiki wangu wataniona kivingine, humo ni full mcharuko,” alisema Kajala. Hata hivyo katika tukio hilo mpemba mmoja aliwavunja watu mbavu kwa kudai atauza hata nyumba yake iliyopo Pemba lakini atahakikisha anamla uloda kuyakomsanii huyo hali iliyowafanya watu kuangua vicheko

MIFUKO YENYE SURA YA BABY MADAH YAANZA KUUZWA NCHINI KENYA, UNAWEZA ICHEKI HAPA



JOKATE "KWA ZAIDI YA MWAKA MMOJA SIJAFANYA MAPENZI

Hii ni mara ya kwanza kwa Jokate Mwegelo kuongelea mambo ya chumban...

Maongezi hayo yalifanyika kati yake na Millard Ayo ambaye ni mtangazaji wa Clouds FM.Katika maongezi hayo, Jokate naye ameeleza jinsi anavyosumbuliwa kutongozwa na mamia ya wanaume kwa siku 


Yafuatayo ni maongezi yao: 

Millard Ayo: Nini kimekufanya ufunguke na hizi info ambazo hujawahi kuzizungumzia na mara nyingi umekua ukigoma kuziongelea kwenye media?

Jokate: Nahisi kwa sababu watu wanazidi kuizungumzia na wanaizungumzia sivyo, hawazungumzii kiuhalisia na kiukweli inanisumbua ndio maana nimeamua kusema kitu kidogo alafu niufunge huu ukurasa.

Millard Ayo: Imekua ikikusumbua kwa mda gani?
Jokate: Kwa muda mrefu, toka mwaka jana… kwenye facebook watu wanatoa comment na najua kabisa watu hawajaelewa hili swala na mimi sipendi mashabiki wangu kutokunielewa.

Millard Ayo: umewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond pamoja na Hasheem?
Jokate: Hahahahahhaha !!!! Yeah..

Millard Ayo: Uhusiano wa nani kati ya hawa wawili ulidumu kwa muda mrefu?
Jokate: Wa Hasheem.. karibia miaka miwili mitatu

Millard Ayo: Na wa Diamond?
Jokate: Oooh kipindi kifupi sanaaa, sijui mwezi sijui miezi miwili… kidogo alinipa tabu, ila kiukweli nilitaka tu kwa sababu kuna watu wengi walikua wanasema Jokate yani vurugu, unajua sio kila kitu unachokisikia ndio chenyewe na media saa nyingine inapenda kuandika vitu ambavyo sio vya ukweli au wanaviwasilisha sivyo.

Millard Ayo: Sasa hivi uko single?
Jokate: Yeah, kwa muda mrefu tu niko mwenyewe alafu saa nyingine wananisumbua sana tena wengi tu, lakini nafurahia kwa sababu naweza kufocus kwenye kazi zangu mfano wiki ijayo nakwenda kushoot movie na JB, muziki na biashara zangu kwa hiyo inanipa fursa nzuri kufanya vitu vyangu, yani mwenyewe kujiamulia asubuhi nakwenda kufanya vitu vyangu hivyo bila kusumbuliwa si unajua Wanaume wanaweza kusema wanataka attention nini… sio kitu kibaya atleast kwa sasa hivi.

Millard Ayo: Umekaa single kwa muda gani sasa hivi? zaidi ya mwaka?

Jokate: Yeah, kwa zaidi ya mwaka mmoja sijafanya mapenzi… sijawahi na mtu ambae nimeweza kumuita like oohh this is my boyfriend… najua ni ngumu lakini nabusubusu watu wengi…. hahah a hah natania hapo, basi tu imetokea hivyo pengine bado sijapata mtu ambae nimeona ataweza kuwa kama wale.

MCHUNGAJI ADAI KUWAUA SHARO, KANUMBA

Kanumba alifariki dunia mwaka jana akiwa nyumbani kwake Sinza-Vatican, Dar huku Sharo Milionea akipoteza uhai kwenye ajali ya gari iliyotokea wilayani Muheza, Tanga wakati msanii huyo akienda kwao mkoani humo akitokea Dar.
Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda.

Stori: Chande Abdallah
Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘The Great’.
Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda.
VIFO MILIONI 605
Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini.
Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao
WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU
Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kundi la Five Stars wapatao 14, Kanumba, Sharo Milionea na mwanamuziki James Dandu ‘Mtoto wa Dandu’.
Pia alidai kuwa alihusika katika vita kati ya aliyekuwa Rais wa Iraq, Sadam Hussein na Marekani kwa kutumia pepo la uchonganishi alilolitaja kwa jina la ‘Magweju’.
Pia mchungaji huyo alidai kuhusika na shambulio la hivi karibuni la Al-Shabaab katika maduka ya Westgate la Nairobi nchini Kenya na matukio mengine mengi hadi kufikia idadi hiyo ya vifo vya watu milioni 605
AWAONEA HURUMA WASANII, AWAONYA
Mchungaji huyo aliendelea kusimulia kuwa alipokuwa katika ulimwengu wa giza aliwahi kuwaonea huruma wasanii kama Kanumba, Sharo Milionea na Mtoto wa Dandu na kuwatokea kimiujiza akiwaonya waokoke kabla ya kuchukua roho zao huku mashabiki wao wakibaki na simanzi wakiamini kuwa vifo vyao ni vya kawaida.
Alidai kuwa baada ya kuwafuata mastaa hao na kuwaonya walikataa na badala yake akawaua.
Akiendelea kulishuhudia kanisa, Mchungaji Mayanga alisema kuwa kwa sasa ameokoka na kuachana na mambo ya giza, hivyo haogopi kuzungumza ukweli kwa kuwa roho wa Bwana anamuongoza kushuhudia kila kitu alichokifanya ili waumini watambue uwezo wa Mungu.
ANA SIRI NZITO ZA VIGOGO
Huku akiomba hifadhi ya majina ya wahusika, mchungaji huyo alihitimisha ushuhuda wake kwa kudai kuwa ana siri nzito za vigogo au watu wakubwa ambao aliwahi kwa namna moja au nyingine kuwapa utajiri wa nguvu za giza.
UTABIRI
Hata hivyo, baadaye jamaa huyo alijitabiria kuwa atakamatwa na kufungwa siku moja kutokana na siri alizonazo.
“Yaani nina siri za watu wengi sana, nikiwaambia mtaogopa na nchi itatikisika. Najua siku moja watu watanikamata na kunifunga pingu kwa siri nilizonazo, lakini kamwe siogopi kwa kuwa Bwana ananiongoza,” alisema Mchungaji Mayanga

EXCLUSIVE : KWA MARA YA KWANZA TAZAMA TATOO MPYAAAAA ALIYOCHORA DIAMOND KATIKA MKONO WAKE WA KULIA

Huenda watu wengi wanaweza wasilishtukie hili, lakini halitaki touch na hii ni kwa mara ya kwanza Unaiona tatoo ya Msanii wa Bongofleva Nasiib Abdul KUPITIA UTAMU WA KITAA hapa hapa,Tumekuleteeni picha hii uiangalie na hii kwa upande wako itakua ni for the first time, Mkono wa kulia wa Diamond Ukiangalia juu ya bega Unaiona Tatoo ambayo sisi bado hutujaielewa imeandikwa vip huenda wewe unaweza kutuambia hapo chini :Hebu icheki then utatuambia:

WADAU WABARIKI NDOA YA WEMA SEPETU, DIAMOND, SASA KAZI KWAO TU

Wadau na mashabiki wa mastaa wawili nchini, Wema Sepetu wa Bongo Movie na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wa muziki wa kizazi kipya, wamebariki ndoa ya wapenzi hao kwa kusema kuwa ni watu wanaoendana na kutegemeana kwa kiasi kikubwa.
Mwanzoni mwa wiki hii, Wema na Diamond walitupia katika kurasa zao za mitandao ya kijamii picha zao, ambazo zinaonekana zilipigwa eneo moja kwa simu moja na hivyo kuwapa wakati mzuri mashabiki wao ambao walionekana kupendezwa na uhusiano wao na kupendekeza waoane.
“Hii ndiyo couple bomba zaidi ya wasanii Bongo, kwa nini msioane? Mnapendeza sana jamani, ebu Diamond Platnumz achana na Penny bwana, huendani naye kwanza kuna mambo ya dini na nini…,” aliandika shabiki mmoja.
Mwingine aliandika: “Nadhani Penny angejiweka tu pembeni awaache hawa wawili, ni mastaa kwa fani zao, yeye angeendelea tu na kazi yake ya utangazaji. Kwanza kwake ni maumivu tu kuwa na msanii ambaye ana shughuli nyingi za kisanii, bora wale wenyewe wanajuana.”
Ingawa kwa muda mrefu Diamond amekuwa akikanusha kurudiana na Wema, hivi karibuni picha zao zilivuja katika mitandao ya kijamii wakiwa China wakila bata na alipoulizwa, ‘alizuga’ eti walikuwa wakitengeneza filamu.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, wadau wengi wanaamini Wema na Diamond wanapendana kwa dhati hivyo wakapendekeza wafunge ndoa na kuyaacha maisha mengine yaendelee kuwepo kuliko kuachana kisha kurudiana mara kwa mara

LULU AFUNGUKA NA KUSEMA KUA HAITAJI KUOLEWA, SOMA HAPA UJUE NI SABABU IPI IMEMFANYA ASEME HIVYO

Muigizaji wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekataa kabisa suala la kuolewa kwa sasa akidai moyo wake haupo tayari kwa tendo hilo.
Lulu alifunguka hayo Jumatatu iliyopita katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa kupitia Runinga ya East Africa ambacho humpa nafasi staa kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake na sanaa kwa jumla.
Wakati mahojiano hayo yakiendelea, mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho anayefahamika kwa jina la Muba, alimtupia Lulu swali ambalo lilimtaka aeleze utayari wake endapo mtu akijitokeza na kutaka kumuoa.
“Sitaki kuolewa kwa sasa, muda wa kuolewa haujafikia. Ukifika nitafanya hivyo lakini kwa sasa sipo tayari kuolewa,” alisema Lulu.
Aidha, Lulu alikiri kuwa licha ya kutokuwa tayari kuolewa lakini amekuwa akipata usumbufu mkubwa wa kutongozwa na wanaume. Aliainisha kuwa alikuwa akitongozwa kabla na baada ya kutoka Segerea alipokuwa akishikiliwa kwa kesi ya kifo cha aliyekuwa mpenzi wake, marehemu Steven Kanumba.
 “Watu wananitongoza sana, walikuwa wakifanya hivyo kabla hata sijaingia China (gerezani Segerea) na wameendelea kufanya hivyo hata baada ya kutoka,” alisema Lulu na kuongeza:
“Siwezi kuwakubalia sababu sipo tayari kuolewa kwa sasa…muda wa kufanya hivyo haujafika.”
Kuhusu suala la kudaiwa kutembea na bosi wa Kampuni ya Proin Promotion ambayo inamsimamia kisanii kwa sasa, Lulu aliruka viunzi na kudai taasisi hiyo inamlea kama mtoto wa familia na siyo vinginevyo.
Alisema hata madai yanayoelekezwa kwake kuwa Proin wamempa gari na nyumba kama sehemu ya kuhongwa na bosi wa kampuni hiyo, hayana ukweli wowote kwani yeye anafanya kazi kama msanii chini ya kampuni hiyo na hakuna kitu cha ziada.
“Hahahaha! Salama (mtangazaji) acha mambo yako bwana… mimi nipo chini ya Proin kwa sasa kwa kipindi flani ambacho nimesaini nao mkataba. Wananilea kama msanii wao, hakuna cha ziada,” alisema Lulu.
Akiendelea kubwabwaja maneno ndani ya kipindi hicho, Lulu aliweka wazi kuwa alikuwa akishindwa kuanika penzi lake na marehemu Kanumba kwa kuwa muda muafaka ulikuwa haujafika na kudai waliishi kama mtu na baba yake kabla hawajawa wapenzi, wakawa wapenzi na mauti yakamkuta Kanumba kabla hawajalianika penzi lao.

LULU ASIMULIA JINSI MIDUME INAVYOMPAPATIKIA USIKU MCHANA...!!

MSANII wa filamu nchini Tanzania Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la (Lulu) ameonyesha kufurahishwa na tukio la wanaume wengi wenye pesa nyingi kumtongoza na kumtaka kimapenzi kila kukicha..

Akizungumza  na  mpekuzi  wetu,Lulu alisema kwamba pamoja na kwamba wanaume wengi wa kila aina na wenye pesa nyingi  wanamtongoza kila siku,  lakini pia anafurahia kupendwa na kwamba anapogundua kwamba anapendwa huwa anajisikia raha na mwenye rufaha zaidi.

"Ninatongozwa  sana  kila  siku  na  wanaume, tena  wenye  pesa  zao.Binafsi  nafurahi   sana  kupendwa  na  ninapogundua  kwamba  mtu  flani  ananipenda  huwa  najisikia  faraja  sana..

"Kutongozwa  kwa  mwanamke  yeyote  mzuri  ni  jambo  la  kawaida.Kukubali  au  kukataa  ombi  la  mwanaume ni  maamuzi  ya  mtu  binafsi. Mpekuzi  naomba  usiniulize  ni  wangapi  nimewakubali  au   kuwakataa  
( huku  akicheka ) 

Akifunguka zaidi kuhusu bahati  hiyo , Lulu   alidai  kuwa hali ya  kutongozwa sana   iliongezeka  baada  ya  yeye  kutoka  gerezani...

"Niliporejea uraiani,  kasi ya kutongozwa ilizidi sana  tofauti  na  nilivyokuwa  nadhani

SHOW YA WEMA SEPETU IMEANZA KUONEKANA KWA TV..!! KAMA UNATAKA KUMJUA WEMA NI NANI, TABIA YAKE, NA MAZURI NA MABAYA ANAYOFANYA BASI SOMA HAPA..!!

Show ya TV ‘In my shoes’ ya mwigizaji Wema Sepetu kutoka bongo movie imeanza kuonyeshwa Eatv October 16 2013 ambapo Episode hii ya kwanza imeanza kwa kumuonyesha Wema kwanza akieleza yeye ni nani, anafanya nini, ni mtu wa aina gani na mengine kama hayo ambapo yafuatayo hapa chini ni maswali aliyoulizwa na kuyatolea majibu.



Swali: Wema ni nani?



Jibu: Wema Sepetu is a girl, i can say a Lady mwenye umri wa miaka 24 kutoka familia ya Isack Abraham Sepetu, a darling, a libra.. a girl who is very ambicious, i love my self…



Swali: Siku yako ya kwanza shuleni ilikuaje?



Wema: Siku ya kwanza tumeenda nikakutana na msichana flani hivi anaitwa Shubira nakumbuka mpaka leo, alikua rafiki yangu wa kwanza tulikutana shuleni nilikua na miaka minne… tumekaa nikaanza kulia kwa sababu ilikua sehemu mpya, mazingira mapya baada ya hapo tukazoea.



Shule ilikua vipi kipindi unasoma?



Wema: Naweza kusema kipindi ambacho niko shule, Mwalimu wangu sijawahi kukaa hata siku moja kumfikiria mara mbili na haijawahi kutokea kwamba hata mwalimu akaweza kufanya labda matamanio au kutaka kitu chochote, hamna kitu kama hicho

Swali: Utafanya nini ikitokea umerudi shule?

Wema: Ningepata nafasi ya kurudi shule, academic nini uniform na nini… ningejaribu kuifanya more fun, a place where everybody can be just himself or herself and just be Wema Sepetu kwa sababu right now this is my time!!

Swali: Ni nani ambae uko karibu nae kwenye familia yenu?

Wema: Dada yangu wa kwanza kuzaliwa anaitwa Tunu, tunakwenda sawa kwenye many many ways, kipindi mama yangu alivyonizaa aliumwa akalazwa hivyo dada yangu ndio akawa ananihudumia kama mtoto wake, ananinywesha uji… anahakikisha nimekunywa maziwa on time na mpaka leo ananiita my baby and I call her my mami… mtu wa pili ni dada yangu wa tatu, she is my bestfriend… baba yangu atabaki kuwa baba yangu tu, mama yangu ni my gurdian Angel, my heart my darling.




Swali: Ulishawahi kugombana na ndugu zako?



Wema: Yeah nimegombana na dada yangu mpaka sasa hivi hatuongei, sio kitu chepesi….



Swali: Unaamini Mama yako ni mkorofi?



Wema: Linapokuja swala la mama yangu huwezi ukasema kwamba ni mkorofi lakini hapendi nikikosea wala kufanya kitu ambacho sicho…. kutokupenda kwake inafikia point anakua na hasira sana alafu njia ya kuonyesha hasira yake ndio level ya juu, yeye anafikiria kwamba anatengeneza ila badala ya kutengeneza ndio anaharibu.


Wema na Mama mzazi



Swali: Wema ni mkorofi?



Wema: Mimi sio mkorofi, mtu ambae hanijui ndio ataniita mkorofi ukishanijua yani tutafika mbali lakini usiponijua na hujui ninachonitaka ndio tatizo.



Swali: Unajisikiaje kuwa Wema Sepetu?



Wema: Kuwa Wema Sepetu sio kitu rahisi, haiwezi kuwa kama watu wanavyofikiria na haitakua hivyo kwa sababu ni maisha ambayo naishi, ni mpaka uone maisha ninayoishi ndio unielewe… yani hata kujaribu kuieleza ili uielewe napata tabu… mashabiki wangu wananielewa sana na uhusiano wangu na wao ni mzuri na ni tofauti na uhusiano kati yangu na familia yangu’




Swali: Unachukulia vipi unaposemwa ama kuandikwa vibaya?



Wema: Katika vitu vyangu ambavyo mtu wa nje anaweza kuviona kama vile… Mungu wangu Wema ana nini, mi navichukulia kama changamoto… mi naona kuna kitu special kuhusu mimi, kwa nini wasiseme watu wengine?



Swali: Unaamini wewe ni mrembo?



Wema: I am beautiful, naamini kwamba mimi ni beautiful kwa sababu nina pure heart… ni kitu Mwenyezi Mungu alichonibariki nacho.

Swali: Kitu gani unachojivunia kwamba kinakutofautisha na wasanii wengine?



Wema: Ninachojivunia… uelewa wangu, I am very very smart.. ni mtu ambae ukiniambia kitu, fasta…. na hata kama sijui kitu, kujiua itanichukua muda mfupi, ability kusimama na kuongea na nikasikika, lugha…. hivyo ni vitu ambavyo najivunia sana



Swali: Unavuta sigara?



Wema: Ndio, ninapokua na msongo wa mawazo sana huwa nafanya hivyo ili kuondoa mawazo na inaweza kutokea mara moja kwa mwezi..



Swali: Ni kweli kwamba wewe ni limbukeni wa umaarufu?



Wema: Sijaacha ustaa uniendeshe, unajua kuna wale watu wanaacha ustaa uwameze mpaka wanabadilisha kuongea, watu wengine wanaacha ule ustaa unawaendesha mwisho wa siku unaanza kuishi maisha ambayo hawana inafika point unaishi kama mtumwa mwisho wa siku unaishi maisha ambayo huna, unaanza kuumia Mungu wangu nimeshazoea kuishi maisha yale, ishi vile ambavyo unaweza… huna pesa, huna! mimi ni mtu ambae ninaweza kuamka nasikia hamu ya kula mihogo, nafanya kitu ninachopenda na sio anachotaka mwingine’



Swali: Gucci na Vanny ni kina nani kwako?



Wema: My precious, kipenzi changu ni Vanny, katakufanya tu ukapende…. Gucci staa anajifanyaga kama yeye mtu tu wa kuchil!



Swali: Unaamini katika ushirikina?



Wema: Ushirikina najua kwamba upo, uchawi kama uchawi upo worldwide ila sipendi kujishirikisha manake sitaki siku moja kuwa mtumwa, mimi mtoto wa Kiislamu nafanya kisomo nachinja kila baada ya muda so naamini ukifanya hivyo unajikinga na vitu vingi.


Swali: Umeshawahi kulogwa?



Wema: Nimeshawahi kulogwa, imeshawahi kunitokea kabisa yani… ni kitu kingine ambacho huwa sipendi kukizungumzia.



Swali: Ulishawahi kwenda kwa Mganga?



Wema: Siwezi kuficha, wamekuja wengi ambao wanataka kunipeleka wengine mpaka kuniletea Waganga nyumbani kwangu lakini Quran mimi ndio mganga wangu namba moja.



Swali: Unafikiri kuna Wasanii wenzako ambao wanakuchukia?



Wema: Unategemea nini once ukishakua katika spotlight, hautegemei kuwa na watu wazuri karibu yako lazima wengine watakua ni wabaya na sio kila mmoja atakua anakuchekea kwa uzuri, wengine sio kutoka moyoni, wanakuchekea tu kwa sababu hawana choice.



Swali: Nani alikua mpenzi wako wa kwanza?



Wema: Sitaki kumtaja bwana….


Swali: Inasemekana unapenda mahusiano ya kimapenzi na watu maarufu?



Wema: Sio kwamba Wema anapenda kuwa na wapenzi maarufu, ni field ambayo tuko, tuko kwenye kiwanda kimoja kwa hiyo kwangu imekua iko hivyo, ni watu ambao mtakua mna interest zinaendana..



Swali: Umeshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu wangapi?



Wema: Wanne, watano au Wanaume sita hehhehe!!



Swali: Mlianza vipi mapenzi na Diamond?



Wema: Tulikua na hii Chemistry inaendana ilikua crazy, baada ya yeye kuniandikia msg kwenye facebook na kuniambia ananipenda, ni mtu ambae nilipata uzoefu mapenzi yanaweza kuwaje, nilipitia kwenye furaha na huzuni nikiwa na yeye…. kilichotokea kimetokea



Swali: Kuna ushindani wowote kati yako na Diamond?



Wema: Once upon a time kulikua na Diamond na Wema, na hawa watu walifall inlove…. watu wanajaribu sana kutulinganisha au tunaonekana tunashindana labda kwa sababu yeye anafanya vizuri kwenye industry yake na mimi nafanya vizuri kwenye industry yangu, mi sijawahi hata siku moja kushindana na Diamond…. mi kuimba siwezi.


Wema na Kajala Masanja



Swali: Kajala Masanja ni nani kwako?



Wema: Kajala ni rafiki, dada…. ndugu ambae hayuko kwenye ukoo wa Sepetu lakini uhusiano wangu na wake kwenye urafiki toka mwanzo sidhani kama nimewahi kuwa na uhusiano huu na mtu yeyote, watu wanadhani kwamba nimeanza kumjua juzi… tokea mwaka 2007 mi nimeanza kumfahamu Kajala mpaka tukawa marafiki sana hadi tunajikuta tumevaa sare.



Swali: Wazo la kumtolea Kajala dhamana ya milioni 13 lilitoka wapi?



Wema: Nilimuangalia Kajala analia pale kizimbani, aidha ilipwe faini au aende jela…. kilikua ni kitu ambacho hakijapangwa, ilikua suprise kwetu wote ila nilichokua nataka ni Kajala kuwa huru kwa hiyo kilichoweza kufanyika kilifanyika.

Swali: Ulijisikiaje siku tatu ulizolala Mahabusu?



Wema: Haikua nzuri kabisa, ni siku tatu mbaya kwenye maisha yangu… hakuna binadamu ambae hapendi uhuru, kwanini nilimsaidia Kajala na kupata nguvu ya kutoa hizo milioni 13? kwa sababu nimekuepo hapo… mimi siku tatu zilikua balaa sasa mwenzangu mwaka mmoja naa? ingekuaje? hata kama nisingemsaidia Kajala alafu Kajala ndio angekaa miaka hiyo 7 sijui 8 jela mimi nisingeweza kuishi, sio Wema Sepetu alivyo’



Swali: Best Werema ni nani katika kampuni yako?



Wema: Bestizzo ni blogger wangu na mpiga picha wangu, anarun kila kitu kinachohusu kampuni kwenye social network Website nini…



Swali: Kwanini uliamua kufanya nae kazi?



Wema: Kipindi cha kwanza niliona kumpa kazi ingeleta matatizo flani lakini nikafikiria, namjua Bestizzo alikua akifanya kazi kwa Diamond na alikua mfanyakazi mzuri, sijui ni kitu gani kilimfanya aondoke kwa Diamond kwa sababu mimi wakati sikua kwenye uhusiano mzuri na Diamond, Best bado alikua kwa Diamond na kipindi hicho hata bado nilikua sijafungua kampuni, hata alikua haniombi kazi ila alihitaji nimuunganishe na wengine’


Tiny Dad na Petit



Swali: Uko vipi na Tinny Dad, Pettman na Martin Kadinda?



Wema: Tiny na Petti ni watu wangu wa karibu sana, nimewajua kwa muda mrefu na wananijua na ninawajua.. Kadinda kabla ya kuwa meneja wangu alikua rafiki yangu, hakua rafiki yangu wa hivyo… tulikua hatuonani hata miezi sita lakini tukikutana namwambia yote yaliyopita, mwaka juzi ndio Martin akasema ngoja niwe Meneja wako, hatukua hata na mikataba mwanzoni… tukajaribisha na tukafanikiwa mpaka leo niko nae.

KUMBE PENNY WA DIAMOND ANATUMIA KITU CHA ARUSHA?.......USHAHIDI HUU HAPA


AUNTY LULU AFUNGUKA MARA BAADA YA KUIBIWA NGUO ZAKE ZA NDANI

MSANII wa filamu za Kibongo aliyeibukia kwenye utangazaji, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amekombwa vitu kibao vya thamani dukani kwake na watu wasiojulikana.

Tukio hilo la kuhuzunisha lilitokea wiki iliyopita, usiku wa manane katika duka la msanii huyo lililopo  Kinondoni – Biafra jijini Dar es Salaam ambapo vitu vilivyoibwa ni pamoja na Chupi zake,  viatu, nguo, pochi, simu na fedha.
 

“Kwa kweli nimechanganyikiwa sana, hadi sasa bado sijajua thamani ya vitu vyote kwa jumla ni kiasi gani lakini nasema sitaki lawama. Walioniibia ni heri wanirudishie tu kwa njia yoyote maana kitakachowakuta hawatasahau.
 
“Nimeshakwenda Bagamoyo kwa mtaalamu wangu na kazi imeshakwisha. Natoa siku saba vitu vyangu viwe vimerudi vinginevyo...” alisema Aunty Lulu bila kufafanua zaidi

KUTANA NA VANITY WONDER MCHEZA SHOW ANAETUMIA ZAIDI YA MILIONI 24 ZA KIBONGO KUONGEZA MAKALIO YAKE




Akiwa amesimama studio za ITV (UK) kuwaonyesha watangazaji umbo lake




Speaking out: Vanity hopes her experience will deter other women from having illegal butt injections

She said: 'Having the infection didn't make me stop. It was only when I was faced with jail and being away from my kids.'
Vanity is no longer a dancer and hasn't had injections since May 2011. She now says she wants to dedicate her life to warning others of the dangers of having illegal injections.
She has written a book, Shot Girls, which charts her own experience of having illegal injections and warns against following her example.
'I wanted to tell the truth 100 per cent so people know what it really is. You can get implants but injections made freely into your butt is not legal in any sense of the word,' she said.

TAZAMA PICHA ZA JINSI BOB JUNIO, MASAI NYOTAMBOFU NA SAMIR WALIVYOTUA TABORA KWA AJILI YA KUPIGA SHOW SIKUKUU YA IDD


Bob Juniour alivyotua ilikuwa TABORA ilikua hivi.

BOB JUNIOUR AKIWA NA MMILIKI WA TABORA REST HOUSE

THE CHOCOLATE; WASHINDI SHINDANO LA DANCE MIA MIA 2013 WAKIWA WAMEFIKA TABORA USIKU HUU KWAAJILI YA SHOO YA SIKUKUU YA EID EL HAJ HAPO TAREHE 16 JUMATANO MWEZI HUU


MASAI NYOTAMBOFU NDANI YA TABORA REST HOUSE-UZUNGUNI BAADA YA KUWASILI USIKU HUU KWAAJILI YA KUPIGA BONGE LA SHOO YA EID EL HAJ NDANI YA UWANJA WA ALLY HASSAN MWINYI KWA MCHANA KWA KIINGILIO CHA 1,000/= KWA MTOTO NA 3,000/= KWA WATU WAZIMA KISHA USIKU NI PALE UKUMBI WA TEKU (ZAMANI DIAMOND TALKIES) KWA MTONYO WA SH 5,000/= TU


SAMIR MZEE WA VINYULINYULI Akiwa mjengoni baada ya kuwasili Tabora.

DIAMOND AWAFUNIKA P-SQUARE KATIKA WIMBO WA TEMPTATION,ANGALIA VIDEO HAPA CHINI....

Mcheki msanii Diamond katika Coke StudioAfrica akiperfom wimbo wa P-SQUARE - Temptation

HUYU NDO ANASADIKIWA KUWA DEMU WA NIKKI WA II

KUTOKANA NA MSANII WA HIP-HOP TOKA ARUSHA KUWEKA PICHA YA HUYU MREMBO MARA KWA MARA KATIKA UKURASA WAKE WA FACEBOOK ,WATU MBALIMBALI WAMETOA MAONI YAO NA KUSEMA HUENDA AKAWA NI MCHUMBA
WAKE ,JAPO KUWA HUWA HAANDIKI CHOCHOTE KUHUSIANA NA HIZI PICHA.


SOMA ALICHO ANDIKA MASANJA MKANDAMIZAJI KATIKA PAGE YAKE YA TWITTER LEO