Showing posts with label michezo_ndani. Show all posts
Showing posts with label michezo_ndani. Show all posts

LEO PATAKUWA HAPATOSHI UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR!! NANI ATAMPAKATA MWENZAKE?..

Watani wa jadi nchini Simba na Yanga leo jioni wanashuka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kupambana katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, huku Simba ikiwa na rekodi nzuri ya kuifunga Yanga mabao 5.

Kila upande umekuwa ukitamba kuibuka na ushindi leo

SIMBA NA YANGA PRESHA TUPU...KOSA MOJA TU KWISNEY

Vinara wa Ligi Kuu, Simba wanafahamu  kwamba, watani zao Yanga wanawasubili kwa hamu wafanye makosa tu wawashushe kileleni.
Simba leo watashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwakaribi Tanzania Prisons kwa lengo moja tu la kupata ushindi ili kuendelea kubaki kileleni.
Mahasimu wao wakuu, Yanga ambao pia leo watateremka Uwanja wa Kaitaba mjini  Bukoba kumenyana na Kagera Sugar, wapo katika nafasi ya nne na pointi zao 12.
Hiyo ina maana kwamba kama Simba itavuna pointi tatu au sare itaendelea kukaa kileleni, lakini kama itapoteza na Yanga kushinda na kufikisha pointi 15 itakuwa imekiweka rehani kiti chake cha uongozi, kwa vile hatima hatma yao itaamuliwa na kigezo cha uwingi wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Pia, Simba inafahamu madhara ya kupoteza mchezo huo hasa baada ya kusakamwa kwa karibu na Azam FC na Mbeya City ambazo kila moja imejikusanyia pointi 14 na kama zitashinda mechi zao zijazo zitakuwa na fursa ya kukaa kileleni.
Kocha wa Simba Abdalah Kibadeni ‘King’ alisema: “ Tupo tayari kwa ajili ya kuikabili Prisons, kwa vyovyote vile mchezo utakuwa na ushindani mkubwa lakini tumejiandaa kwa ajili ya kuhakikisha tunaibuka washindi.”.
Naye Kkocha wa Yanga,Ernest Brandts alisema: “Wachezaji wangu wote wapo katika hali nzuri wakiwa na morali kubwa ya kuhakikisha wanashinda.” Kwa upande wake, Kocha wa Prisons, Jumanne Chale alisema: “Simba ni timu ya kawaida kama zilivyo timu zingine,
hatuihofii wala kuigopa, baada ya dakika tisini nina uhakika matokeo mazuri yatakuwa upande wetu”.
Kocha Msaidizi wa Kagera, Mlage Kabange alisema: “Nadhani hakuna namna ambayo Yanga wataepuka kipigo, vijana wangu wamepania kuendeleza ubabe kama ilivyoku wenye Uwanja wa Azam Complex vibonde wa ligi hiyo, Ashanti United wataivaa Coas tal Union.

GARI YA BILIONEA ANAYEMILIKI MANCHESTER CITY YAONEKANA DAR, ANAIMILIKI YUSSUF BAKHRESA


Gari aina ya Brabus ambayo inayomilikiwa na mmiliki wa klabu ya Manchester City ya England, imeonekana leo Dar es Salaam, lakini ni mali ya Yussuf Bakhresa, mtoto wa bilionea Mtanzania, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa. Vyanzo vimesema Yussuf alitoa oda maalum kutengenezewa gari hili na thamani yake jumla si chini ya dola za Kimarekani 500,000.

Hii hapa mali ya Yussuf Bakhresa

Huyu jamaa ndiye anayeendesha gari la hili la mtoto wa Bakhresa

Angalia alivyotulia ndani ya mzigo wa dola 500,000

Ni oda maalum kwa ajili ya Yussuf Bakhresa 



Kutoka Manchester hadi Dar es Salaam

TAZAMA PICHA ZA AZAM TV WAKIWA KAZINI KATIKA UWANJA WA TAIFA.

AZMA TV imeanza kuonyesha mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Kituo cha TBC1. ambapo meci ya kwanza ilikuwa ni mchezo kati ya Simba na Ruvu Shooting, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Picha nyingine ni baadhi ya wafanyakazi wa Crew ya AZAM TV wakiwa kazini ndani ya Uwanja wa Taifa.




WATZ WAZUNGUMZIA SOCCEREX AFRICAN FORUM 2013,FUATILIA

Jukwaa lilioandaliwa na SOCCEREX kwa ajili ya kuzungumzia mambo kadhaa wa kadhaa yanayolihusu soka la Afrika pamoja na mianya ya kibiashara iliyopo limemalizika leo hii jijini Durban nchini Afrika Kusini.

Washiriki walitoka kila kona ya bara la Afrika na wengine walitoka nje ya bara la Afrika lengo likiwa ni kusikiliza mada mbali zilizokuwa zikitolewa na wazungumzaji mbali mbali kuanzia wafanyabiashara,viongozi mbali mbali wa mpira wa miguu,Wadau wa mchezo huo bila kuwasahau Mawaziri na viongozi mbali mbali wa Serikali.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizotoa wawakilishi kwenye hilo jukwaa,Mheshimiwa naibu waziri wa Habari,kazi vijana na Michezo ndugu Amos Makalla aliwaongoza watanzania wachache walioshiriki kwenye semina hiyo.
Watanzania wengine walioshiriki kwenye semina hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Azam FC ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa kamati ya ligi ndugu Said Mohammed,C.E.O wa kamati ya ligi ndugu Silas Mwakibinga bila kumsahau mmiliki na meneja mkuu wa African Lyon ndugu Rahim Kangezi.

Mara baada ya semina hiyo kumalizika washiriki hao walikuwa na haya ya kusema.

Silas Mwakibinga- C.E.O wa kamati ya ligi:

''kwanza nimegundua bado tuna safari ndefu,tuna mambo mengi ambayo tunapaswa tuyafanyie kazi kutokana na maada nyingi zilizozungumzwa na wazungumzaji mbalimbali,Binafsi nimevutiwa sana na mipango ya raisi mpya wa SAFA Dr Danny Jordaan alivyokuwa akizungumzia takwimu za kiufundi kuhusu nchi yake,nimevutiwa sana kusema ukweli takwimu zile alikuwa anazitoa kichwani bila kutumia karatasi na zilikuwa zinaonekana kabisa ni za na mtu ambaye ni mtendaji,akizungumzia
idadi na uwiano wa makocha wanaowalenga,uwiano kati ya makocha na wachezaji,wanatakiwa kuwafundisha makocha wa kila madaraja wangapi kwa mwaka na kutaka kuuendeleza mpira kuanzia ngazi za chini mpaka juu hiyo inaonyesha baada ya uwekezaji huo kufanyika nchi hii itabadilika sana kimpira,amezungumzia mpango wa nchi nzima wa kuzalisha idadi ya wachezaji pia mfumo wa kuchezwa kwa ligi za watoto nchi nzima,kwakweli nadhani haya mawazo yanafaa kuigwa na sisi viongozi wa mpira katika nchi yetu,lakini pia nimevutiwa na raisi wa chama cha soka cha Ghana Kwesi Nyantakyi alivyokuwa akielezea namna ambavyo vilabu vyenye madeni haviruhusiwi kucheza ligi nchini mwake''

SAID MOHAMMED-MWENYEKITI AZAM/MAKAMU MWENYEKITI KAMATI YA LIGI:

'Semina hii imetusaidia kutufungua macho hasa katika mipango ya kibiashara inayotokana na mchezo wa soka,kuna vitu tulikuwa tunavifahamu lakini hatukujua namna ya utekelezaji wake,semina hii pia imetusaidia kutupatia mawasiliano na wenzetu toka nchi mbali mbali kama vile Nigeria,Ghana na Kenya ikiwa ni pamoja na kutupa mbinu za namna hawa wenzetu wanavyoendesha ligi zao''

RAHIM KANGEZI- MMILIKI AFRICAN LYON:

''Vitu vingi sana vizuri vimezungumzwa lakini bila kuheshimu proffesionalism ichukue mkondo wake kamwe hatutapiga hatua,nimefurahishwa na mpango wa miaka 10 wa maendeleoya soka nchini Afrika Kusini,mpango unaonyesha namna ya kuwatafuta vijana wenye vipaji,lakini pia unavyozungumzia mfumo wa mashindano ya nchi nzima,namna ambavyo wataboresha miundo mbinu pamoja na teknolojia watakayoitumia ili kuhakikisha mipango yao inafikiwa,hilo kwa kweli limenipa matumaini makubwa''