AUNTY LULU AFUNGUKA MARA BAADA YA KUIBIWA NGUO ZAKE ZA NDANI

MSANII wa filamu za Kibongo aliyeibukia kwenye utangazaji, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amekombwa vitu kibao vya thamani dukani kwake na watu wasiojulikana.

Tukio hilo la kuhuzunisha lilitokea wiki iliyopita, usiku wa manane katika duka la msanii huyo lililopo  Kinondoni – Biafra jijini Dar es Salaam ambapo vitu vilivyoibwa ni pamoja na Chupi zake,  viatu, nguo, pochi, simu na fedha.
 

“Kwa kweli nimechanganyikiwa sana, hadi sasa bado sijajua thamani ya vitu vyote kwa jumla ni kiasi gani lakini nasema sitaki lawama. Walioniibia ni heri wanirudishie tu kwa njia yoyote maana kitakachowakuta hawatasahau.
 
“Nimeshakwenda Bagamoyo kwa mtaalamu wangu na kazi imeshakwisha. Natoa siku saba vitu vyangu viwe vimerudi vinginevyo...” alisema Aunty Lulu bila kufafanua zaidi