Ngoma ya Gosby, Baby Makinga aka BMS umeweka historia ya Tanzania kwa kuwa miongoni mwa nyimbo pekee kutoka Afrika Mashariki kuweza kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuingia kwenye(mixtape) namba 1 duniani, ya Coast2Coast Vol 251 ya nchini Marekani.
Hadi sasa, BMS inashika nafasi ya 9 kati ya nyimbo 40 zilizoingizwa kwenye kinyang’anyiro hicho ambapo nyimbo 20 tu ndizo zitakazopata fursa ya kuingia kwenye mixtape hiyo. Fursa hiii tampaGosby nafasi ya wimbo wake wa BMS kusambazwa kwa wadau na wapenzi wa muziki zaidi ya 2,000,000 duniani.
Kwa kushika nafasi ya 9 ni kwamba Gosby tayari ameshaingia kwenyemixtape ya coast2coast lakini kura zaidi zinahitajika ili aweze kuendelea kukaakileleni au hata kufika nambari moja. Mwisho wa kupiga kura ni October 8.
Coast2coast ni nini?
Coast2Coast ni kampuni ya kimarekani inayojishughulisha na usambazaji na promosheni za mixtapes duniani.
Coast2Coast mixtapes ni mixtape zinazokuwa downloaded kwa wingi zaidi duniani na zimepata zaidi ya downloads Million 200 tangu zilipoanzishwa miaka kadhaa iliyopita.
Coast2Coast mixtapes ni mixtape zinazokuwa downloaded kwa wingi zaidi duniani na zimepata zaidi ya downloads Million 200 tangu zilipoanzishwa miaka kadhaa iliyopita.
Miongoni mwawasanii ambao wameshawahi kufanya kazi na coast2coast mixtapes ni pamojana 50 cent, Snoop Dogg, Wiz Khalifa, Big Sean, Game, Pharrell, Nas, Lupe Fiasco, Chris Brown, LL Cool J, Fabolous, Gym Class Heroes, Flo Rida na wengine wengi. Vile vile madj kama Dj Drama, DjKhaled, Bigga Rankin, Dj Ill Will na wengine wengi.
Kila toleo la mixtape za Coast2Coast husambazwa kwa watu zaidi ya million 2 duniani na hupostiwa kwenye zaidi ya websites/blogs 1000 maarufu za muziki duniani ambazo kwa ujumla hupata downloads zaidi ya 500,000 kila toleo. Vilevile kila toleo husambazwa na wasambazaji zaidi ya 400 ambao husambaza copies katika majimbo kadhaa nchini Marekani, Africa na Ulaya.
JINSI YA KUPIGA KURA
Ingia kwenye link hii http://coast2coastmixtapes.com/audiodetail.aspx?audioid=270668
Katikati mkono wako wa kulia utaona neno VOTE by FACEBOOK or TWITTER kama uko facebook basi piga kura yako kwa FACEBOOK na kama uko TWITTER piga kura yako kwa TWITTER.