HIZI NDO VURUGU ZILIZO TOKEA JANA MVOMERO MKOANI MOROGORO KATI YA WAKULIMA NA MAFUGAJI, TAZAMA HAPA

Gari la mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero likiwa nje ya kituo cha polisi Dakawa.
Vurugu za wakulima zimezuka tena Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ,ambapo kundi la wakulima limefunga barabra ya Turiani-Morogoro eneo la Mkindo wakipinga wafungaji kuchoma nyumba kadhaa za wakulima sambamba na kushinikiza serikali kuwaruhusu kulima kwenye bonde la Mgongolwa.Katika vurugu hizo wakulima hao walirusha mawawe yaliyosababisha Polisi mmoja kukimbizwa hospital baada ya kupigwa jiwe kwenye paji la uso huku gari la mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero likihalibika vibaya baada kupigwa mawe na wakulima hao. 


Askari wa jeshi la Polisi akikagua gari la mkurugenzi lililoaribiwa vibaya katika vurugu hizo

waandishi wa habari wa waliofika eneo la tukio pia walipigwa mawe na wakulima hao na kushindwa kutekeleza majukumu yao na kuamu kuondoka eneo hilo la tukio.Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bw Anthony Mtaka alilaani kitendo kilichofanywa na wakulima hao na kulipongeza jeshi la polisi kwa kutumia hekima kwenye vulugu hizo licha ya kupigwa mawe na wakulima hao 


Kundi la polisi wa kutuliza ghasi kutoka moorogoro mjini likieleka eneo la tukio