Jennifer Lopez kuigiza kama mama wa Rihanna kwenye movie mpya

Jennifer Lopez ameongezeka kwenye orodha ya waigizaji kwenye filamu mpya ya animation ya kampuni DreamWorks iitwayo Home, itakayotoka mwakani.


Superstar huyo ataingiza sauti kwenye filamu hiyo kama mama wa Rihanna ambapo imetokana na kitabu cha “The True Meaning of Smekday,” cha mwaka 2011.

Home itaingia sokoni November 2014. DreamWorks iliyoanzishwa na Steven Spielberg magwiji wa filamu za animation ambapo kazi zao ni pamoja na Shrek, Madagascar, Kung Fu Panda, Monsters vs. Aliens na and How to Train Your Dragon.