Msanii mkongwe katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes akiwaimbisha mashabiki wake kibao waliofurika vilivyo ndani ya uwanja wa Majengo mjini Moshi ambapo tamasha la Serengeti fiesta linafanyika.
Kundi la Weusi likiongozwa na Joe Makini wakilishambulia jukwaa usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Mwanadada aliyewahi kufanya vyema kwenye shindano la BSS,Menina akiimba kwa hisia jukwaani
Mkali mwingine wa bongofleva anaefanya vyema kwenye muziki huo,akitambulika kwa jina la kisanii Ney wa Mitego akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye wakati wa tamasha la serengeti fiesta likiendelea kwenye uwanja wa Majengo,mjini Moshi.
Mwanadada Linah akimpagawisha shabiki wake vilivyo jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Mkali wa shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta ndani ya uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Nigeria Jay Martins akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa Moshi waliofika kwenye tamasha la fiesta ndani ya uwanja wa Majengo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye amekuwa akifanya vyema tangu aibuliwe na Serengeti supa Nyoya kutoka jijini Mbeya,Neylee kwa sasa anakula matunda ya ufanisi wake wa kisanii katika anga ya muziki huo,pichani akiwa kwenye jukwaa la serengeti fiesta usiku huu mjini Moshi kwenye uwanja wa Majengo ambapo tamasha hilo likiendelea.
Pichani kati ni msanii wa bongofleva kutoka nyumba ya vipaji THT,Ally Nipishe akiwa na madansa wake wakilishambulia jukwaa la fiesta usiku huu.
Mashabiki waliofika kiwanjani hapo
Mwanadada aliyewahi kufanya vyema kwenye shindano la BSS,aitwaye Menina akiimba jukwaani na madansa wake.
Wasanii wanaounda kundi la Jambo Skwadi wakilishambulia jukwaa kwa namna ya kipekee kabisa usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta linalofanyika kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Msanii wa Bongofleva,atambulikae kwa jina la kisanii AY,akiwaimbisha wakazi wa mji wa Moshi waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,lilofanyika ndani ya uwanja wa Majengo,ambapo pia mwanamuziki maarufu kutoka nchini Nigeria Jay Martins alitumbuiza pia
Shilole kama kawaida
Shilole akiwa kazini baada ya kutoa mwaliko wa kudance na shabiki
Juma Nature na timu yake..
Chege na Temba walifanya yao
Godzilla…
Kasim akifanya yake
Young Killer Mwanza Mwanza
Stamina…
Mr.Blue akifanya yake jukwaani....
Mwana FA
Dully....
AY