Hii hapa tena..!!! Mitaa yetu ya Uswazi siku hizi tofauti na zamani, motto asipokwenda shule basi mtafute kwenye mabanda ya video, siku hizi chaka la kutega shule ni Play Stations.
Tusipoangalia ziro zitazidi kuongezeka kutokana na Play station kutawala vichwa vya watoto wetu. Sheria za biashara hii zitungwe, zisimamiwe kikamilifu na wakosaji wawajibishwe bila uonevu wala rushwa ndani yake