Showing posts with label mahusiano. Show all posts
Showing posts with label mahusiano. Show all posts

SIFA 15 ZINAZOMFANYA MWANAMKE KUMPENDA MWANAUME.

Pengine watu wengi wamekuwa wakitafuta ni jinsi  gani wanaweza kupendwa na wasichana au wanawake. Niwazi kabisa kila mwanamke anachaguo lake kwa mwanaume ampendae.Huenda ukawa unavigezo kibao lakini akapenda mweyevigezo vichache. Vifuatavyo ni vigezo 15 ambavyo wasichana wengi hupenda kutoka kwa mwanaume.
1. Kujiamini
2. Mcheshi
3. Mwenye utashi
4. Anayetoa msaada unapohitajika
5. Anaetunza siri
6. Mwenye kujithamini
7. Mwenye malengo / makini  

8. Mwenye mawazo mapana 
9. Muwazi na mkweli    
10. Anayeridhika        
11. Aliyeshupavu na jasiri
12. Mwenye huruma 
13. Anaesamehe 
14. Hadhi na heshima 
15. Hisia ya uadilifu.

NJIA ZA KUTONGOZA MWANAMKE AKAKUPENDA MILELE..!!!!!!

Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila kumvutia mwanamke yeyote.
Hapa kunanjia 15 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo ;

1. Wakati ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu kumbu yako ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla.
2. Wanawake huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu na kamwe usimpe nafasi ya yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa ukizungumzia.
3. Kuwa makini wakati unapokuwa ukizungumza nae huku akikupatia majibu yasiyo na hisia zozote za mapenzi. Hapo utajua kunakitu, hivyo kama kwa bahati mbaya uko nae karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni wakati ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko sawa katika utoaji majibu.. kwa kawaida atakuonyesha ishara, hivyo kuwa nazo makini.
4. Kumbuka hii kauli mbiu "Ucheshi/vituko si mapenzi". Wanawake huvutiwa sana na wanaume wanaoweza kuwafanya wawe na furaha muda wote. Usijikite zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa unaongea. Bali jikite zaidi katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na msisimko na starehe wakati ukonae.
5. Zama katika undani wa mazungumzo baina yako na yeye. Mwanamke huendana na mwanaume asiyekuwa muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa ukaribu.
6. Wanawake wengi hupenda kujua maoni yako kuhusiana na jinsi unavyomuona. Mwambie vitu unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa makini ili usitamke vitu vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha.
7. Epuka kumpa ofa nyingi mwanamke, mwanamke huwa na mashaka na mwanaume anayempatia vitu vingi kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu atafikiri vitu unavyompatia ni kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi. Kitu ambacho baadae kitaleta madhara makubwa.
8. Kama unahitaji kujua njia nzuri ya kuweza kuongea na mwanamke au msichana bila kumfanya asikudharau au kuboreka, basi usitumie njia ya kumuuliza  maswali mengi katika mazungumzo yenu. Bali jaribu kueleza mawazo yako kuhusu vitu flani.
9. Kumbuka kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza "wewe umekulia wapi?", uliza "unaonekana kama hujakulia maeneo haya!" Hii itakusaidia wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.
10. Usifiche utambulisho wako - zungumza vitu kutoka katika hisia zako, onyesha uhalisia wako katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu yeyote.
Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni kutambua njia sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda kuitumia, isipokuwa usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke sii vigumu bali nikujua ni vitu gani hasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake...kisha rudi toa maoni yako hapa.

MUHIMU: Maelekezo haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye kuhitaji mapenzi ya kweli - yani sio kwa wanawake wanaolenga kuchota pesa kwako na kutokomea. Hivyo kuwa makini sana.

AINA 10 YA WANAWAKE WANAOPENDWA NA WANAUME!!!!!!!!!!!......

WENYE MSIMAMO

Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, walio makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio. 
 
WAPENDA USAWA
 Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50. 

WANAOJUA MAPENZI 
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.

MARAFIKI 
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani. 

WAPENDA UWAZI 
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na wapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo. 

WANAOJITEGEMEA 
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina ‘naomba vocha’ kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja. WASIO NA PRESHA Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi. 

MARIDADI 
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini pia ni waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano. WANAORIDHIKA Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke. 

WA MMOJA 
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana."

MAMBO YANAYOMFANYA MTU AYACHUKIE MAPENZI

SIJUI wewe ulikuwa una malengo gani wakati unafikiria kuwa na ambaye unaye; wapo ambao walikuwa na malengo kwamba akiwa na mwanaume, maana yake awe ndio sawa na mashine ya kutolewa fedha maarufu kama ATM. 

Ikiwa ulichokuwa unatafuta ni mwanaume au mwanamke ambaye kwako atakuwa ni ATM, kwamba ndiye awe anakupa kila kitu unachotaka, ikiwa hatakuwa na fedha si rahisi mkaendelea kuwa na uhusiano mzuri, kwa kuwa mpango wako haukuwa mapenzi, bali kuchuma fedha na kula raha.
 
Wajinga ni wale ambao wanaingia kwenye mapenzi ili kusaidiwa tu, badala ya kusaidiana. Mwenye hekima ni yule ambaye anafahamu kwamba kuingia kwenye mapenzi, maana yake ni kuongeza timu ya kusaidiana katika maisha, si vinginevyo.

Mwanamke yeyote ambaye anafikiri yuko na mwanaume maana yake ni kwamba awe anamnunulia kila kitu, kwamba kwake mwanaume ni kila kitu, kinywaji anunuliwe, chips anunuliwe nk...kwamba yeye ni mtu wa kupewa tu ofa, maana yake ni kwamba akili yake imekufa.
 

Kufikiri kwamba kuoana na fulani maana yake ni sasa yeye atakuwa anakusaidia kila kitu milele na kwamba asipofanya hivyo utamdharau, si kitu sahihi.
 
USIWE NA MATARAJIO MAKUBWA UNAPOINGIA KWENYE NDOA 

 Unapoingia kwenye ndoa, usiwe na matarajio makubwa sana mazuri. Jambo unalopaswa kufahamu ni kuwa uhusiano ni suala la kawaida, kwamba unakuwa na mtu kwa lengo la kuwa nae kama timu moja kusaidiana katika kuleta maendeleo.

Kati ya mambo yanayofanya watu kutofurahia mapenzi, ni pale anapotishwa kwamba labda asipofanya hiki kwa mfano kukusaidia, basi uhusiano wenu utaharibika.
 

Kuna wanawake utasikia aaah sasa kuna maana gani ya kuwa na mwanaume ikiwa namwomba fedha hawezi kunisaidia? Fikra kama hii ni ya kipuuzi. Wewe kwanini huna fedha? Ndoa ni kusaidiana, sio kugeuzana ATM.
 

YUKO BIZE NA SIMU, KOMPYUTA NK
Kati ya mambo yenye kutiana ‘kichefuchefu’ katika mapenzi ni pale kwamba uko na mwenzi wako, lakini ni kama wewe ni tambala la deki; yaani yuko bize na simu yake au kompyuta au kitu kingine chochote.

Wengine unakuta labda anawasiliana na wengine kwa mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter nk, kumaanisha kwamba wewe ni muhimu, walio muhimu ni wale ambao anawasiliana nao huko.
 

KUKOSOANA MBELE ZA WATU AU HATA KUPIGANA
Wapo watu wamekuwa na tabia ya kukosoana au hata kupigana mbele za watu. Kati ya makosa yenye kukera na huenda ukasababisha uhusiano ukabaki historia ni hii...ni vizuri ndugu yangu kujifunza namna ya kuachana na hasira kali.

MATUMIZI MABAYA YA FEDHA NA KUTOKUWA NA MIKAKATI KATIKA MAISHA
 
Kila mtu Duniani anataka maisha bora, kwa maana hiyo ni furaha ya kila mtu kuona mwenzi wake anakuwa mwenye mikakati imara katika kuimarisha maisha yao.


Tabia kama za ufujaji wa fedha, kutokuwa na mikakati katika maisha, ni kati ya mambo yanayochangia ndoa au uhusiano wa mapenzi kuwa mbaya.

HUDUMA KWA WATOTO NA FAMILIA


Ukiwa kama baba au mama, unapaswa kutafakari vizuri nafasi yako katika malezi ya familia. Ni furaha ya mke na mume, kuona mwenzi wake anajali watoto na familia kwa ujumla. Je, wewe ukoje? Pata muda kufakari hali ya maisha yako, chukua hatua. 

UCHAFU NA KUTOWAJIBIKA 


Kuna watu wamekuwa wachafu kupindukia, hata kuoga kabla ya kulala ni shida, wengine kuvaa nguo mpya ya ndani hadi awe na ahadi ya kuonana na nesi au daktari. 

Lakini zaidi ya yote, ni muhimu wanaume na wanawake wakafahamu kila upande kwa kawaida huwa na nafasi yake ya kuwajibika. 


Hata kama wote mna ajira au fedha, mume anapaswa kuangalia namna ya kumfanyia mkewe mambo kama kununua nguo, chakula ndani nk...kuna wanaume hawa hawajui wake zao wamevaa nini wala hawajui ndani chakula kinanunuliwaje...hili ni kosa. Ndoa ni kusaidiana, kila upande uwajibike, ni nzuri kuwa na vikao vya namna ya kuendesha ndoa yenu.

HAYA HUWAFANYA WANAWAKE KUSITA KUINGIA KATIKA NDOA (KUOLEWA)

Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume. Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi.

Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa)

Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake wengi hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe mume wake. Wanawake hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe nazo.  Vigezo hivyo huwa hata kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao hutaka mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua, mtanashati, sauti nzuri n.k. Inaweza kuwa kama mzaha na ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna wale ambao anaweza kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume hafananii vile ambavyo yeye anataka mumewe awe.

Kutaka mwanaume tajiri
Kuna wanawake ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule ambaye hana pesa nyingi. Yupo tayari kuolewa ila si kwa mwanaume mwenye uwezo wa kawaida – hata ikitokea mwanaume ana uwezo kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado huona huyo mwanaume hamfai hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi ataishi maisha ya kifahari. Hivyo hukazana kusubiri na kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume ambaye atakuwa na uwezo mkubwa, bila kujalisha kama huyo mwanaume kampita sana umri.

Kutompata Mwanaume Ampendae
Hili ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani na haifai bali tu hadi pale umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini anakupenda pia.  Wengi katika kundi hili huamini kuwa mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni kupendana tu na mengine hufuata kwenye sababu ya upendo. Kuna wanawake vigezo vya mwanamme awe vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa. Yeye kikubwa anataka ampate mume ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na matumaini kuwa huyo mume atampenda na yeye pia kwa dhati.  Huyu mwanamke anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanaume akampenda ndipo atakapokuwa tayari kuolewa.  

Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa
Kuna wale wachache ambao akili hubadilika kama kinyonga; wasioridhika wala kujitambua ni nini wanataka ama mwanaume wa aina ipi wanataka. Akija wa mwenye uwezo atasema nataka wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo atatoa sababu tu hata kama kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta maendeleo. Akija wa kabila hii, atasema hapana hao wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi ni mtu asiyeisha kutoa kasoro za wale ambao wanajitokeza kutaka kumuoa. Hatimaye inaweza tokea muda wa kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji lakini ikiwa hata wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena katika soko. Kujiona ni mzuri sana
Kuna wanawake ambao ni kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni mzuri kiasi kwamba wake kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na hata wote kumtamani. Hata hivyo hapo hapo kuna wale ambao huwa ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamo wake hujiona ni mzuri mno hakuna mfano kama yeye; kitendo ambacho kwa wachache kwenye kundi hili hufanya kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu anatakiwa atambue kuwa ana bahati sana. Kitendo hiki hukuza nyodo za hali ya juu ya mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi kwamba wanapojitokeza wanaume kutaka kuoa – anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau na kiburi.

Kujiona ana Umri mdogo
Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa. Wanawake wametofautiana mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri wa kuolewa hutamani sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa wakiwa wakubwa zaidi. Katika kundi hili umri kuwa mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka 25 na bado akajiona mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona ni mkubwa na anafaa kuolewa. Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa. Anapokuwa na umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo kwake kuingia katika ndoa.

Maradhi hasa UKIMWI
Hili kama lilivyo kwa wanaume -  Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na mtoto.  Wengi sana hukata tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya hudhoofika zaidi.

Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo maisha ya tamthilia yawe na kwao pia. Hilo linafanya vigezo ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume kumuoa kutotimiza yale ambayo yeye binafsi anatarajia.  Wengi hushindwa kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya maigizo yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo.

Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:
- Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na mengine mengi.
- Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe (pengine mama aliteswa sana), na hata ndugu wa karibu kama vile kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha ya taabu na kuonewa. Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya lolote lile ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama mume kwake anaona kama ni utumwa. Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna wanawake wale wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile ya kimwili ya kuweza kupata hisia za kuweza kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi. Wengi wa aina hii ya wanawake huwa ni waoga sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi hata jaribu baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na uchafu.  Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.

UKWELI USIOPINGIKA KUHUSU UHUSIANO WA WEMA NA DIAMOND,WABONGO WALIUPENDA SANA..CHEKI HAPA

WACHUMBA wa zamani, Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiyo habari ya mjini kwa sasa, kwamba wawili hao wamerudiana tena kwa kasi kupita ile ya mwanzo, Amani limechimbua.
Habari zinasema wawili hao walikutana Dubai hivi karibuni  kabla Diamond hajaenda Malaysia na Wema akiwa njiani kuelekea Hong Kong, China ambapo walikula bata kwa sana.
Ikazidi kuelezwa kuwa wameamua kuwa kwenye uhusiano wa siri na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mpenzi wa sasa wa msanii huyo wa Bongo Fleva, Penniel Mungilwa ‘Penny’ hajui kitu chochote.

TAARIFA ILIVYO
Kwa muda wa siku nne, ndani ya mitandao ya kijamii hasa kwenye Instagram, maneno yenye kuashiria kuwa wawili hao wapo pamoja tena yamekuwa yakichukua nafasi.
Baada ya kusambaa kwa habari hizo, Penny naye alitupia picha yake akiwa kitandani na Diamond na kuandika kuwa waachwe kama walivyo.
Ndani ya mtandao wa Instagram yakazuka makundi mawili, upande wa mawifi wa Penny, akiwemo Halima Kimwana na kundi lingine la mawifi wa upande wa Wema.
Kundi la Wema waliandika kuwa mwanamke anayependwa na ndugu wa mume siku zote mwanamme huwa hampendi hivyo Wema ni mpenzi sahihi wa Diamond kwa vile hapendwi na ndugu kama Penny.

MBAYA ZAIDI
Mbaya zaidi, katika hali isiyotegemewa kwenye akaunti yake ya Instagram, Wema alitupia wimbo mpya wa Diamond uitwao My Number One na kuweka maoni yake kwamba anaupenda wimbo huo.
Wengine waliochangia walisema Wema ana lake jambo kwa Penny kwa vile si jambo jepesi kusifia wimbo wa mwanamme ambaye alikuwa mpenzi wake na sasa ana mwingine anayejulikana, yaani Penny.

PICHA YA WEMA SASA
Wema hakuishia kuposti wimbo huo tu, alikwenda mbele zaidi kwa kutupia picha yake yenye pozi tamu na kuuliza; huyu hapa baby wa nani huyu? (yaani yeye).
Wengi walimsifia lakini wengine walifunguka kwa kusema ni baby wa Diamond, jambo ambalo Wema hakulipinga.

PENNY AONGEA NA AMANI
Kufuatia kuenea kwa habari hizo, Amani lilianza kuwasaka watu watatu ambao ndiyo wenye uwezo wa kubainisha ukweli au uongo wa ishu hiyo iliyoenea mjini.
Watu hao ni Diamond mwenyewe, Wema anayedaiwa kurudiwa na Penny, mpenzi wa sasa wa Diamond.
Wa kwanza kupatikana alikuwa Penny ambapo alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa madai hayo alifunguka:

AKIRI KUNYETISHIWA
“Ni kweli hata mimi nimenyetishiwa habari hizo lakini siamini kama inawezekana hao watu wakarudiana.

ASEMA KUNA KUNDI LINAPANGA NJAMA
“Nijuavyo mimi kuna kundi la watu ambao wapo upande wa pili (wa Wema) ndiyo wanaoeneza hizo habari, pengine wanataka niamini kisha nimwache Diamond, simuachi ng’o.

ANATAKA USHAHIDI 
WA PICHA
“Kama niliweza kumvumilia kwa kuona picha akiwa na Irene Uwoya hotelini sembuse hili la safari hii hata picha hakuna?”

ALISHAMUULIZA DIAMOND
“Mimi nilishamuuliza Diamond, japo hakusema ni kweli au uongo ila aliniambia achana na hizo habari.”

DIAMOND APIGA KIMYA
Baada ya kuongea na Penny, 
 lilimpigia simu Diamond ambapo alipokea na kusema yuko kikaoni na kumtaka paparazi kupiga baadaye. Hiyo ilikuwa saa 4:16 asubuhi ya juzi.
Saa 7:11 mchana, Diamond alipigiwa simu tena lakini hakupokea. Akatumiwa meseji ya kumkumbushia, hakujibu. Akatumiwa meseji yenye madai ambayo pia hakuijibu.

MAMA WEMA KABLA YA KUULIZWA AFUNGUKIA MADAWA YA KULEVYA 
Amani liligundua Wema bado yupo Hong Kong hivyo liliamua kumpigia simu mama yake, Bi. Miriam Sepetu ili kuomba namba ya bintiye, lakini kabla ya ombi hali ikawa hivi:
“We nani, hivi kuna gazeti moja limeandika eti mwanangu amekamatwa na madawa ya kulevya China anasubiri kunyongwa, ni akina nani wale, wana akili kweli?
“Mimi sikubali safari hii, tutafikishana kwa mwanasheria wangu. 
“Tena ukikutana nao waambie waache kumzushia mwanangu, wasimtie mkosi bure, hajakamatwa yupo salama kabisa.” 
Mpaka sasa ushahidi wa kuonesha wapenzi hao wa zamani kuwa  wamerudiana bado haujawekwa hadharani.

GPL