YOUNG DEE AKANUSHA SKENDO YA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

Msanii Young Dee amekanusha uvumi ulioenea mitaani kuwa anajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na kusema kuwa pamoja na story hizo kuwa kubwa lakini hali hiyo haijamuathiri sana kwasababu hazina ukweli wowote.

“Ni story ambazo zimekuwa kubwa sana lakini hazijaniathiri sana kwasababu sio ukweli, lakini zimenifanya nimezidi kuwa makini sana kuwa muoga pia na vitu vingi sana kuangalia watu wanaonizunguka, mazingira na vitu kama hivyo”.
Alisema Young Dar es salaam kupitia E-News ya EATV jana . 
Dee amesema kuwa anafahamu fika kuwa utumiaji wa ‘unga’ unaweza kuathiri kazi yake ya muziki kutokana na mifano hai ambayo imeshaonekana kwa wasanii wengine, 
“The more the story zinakuwa kubwa zinapoteza maana nzima ya kitu nachohangaikia kila siku ambayo ni muziki, so naonekana muziki nafanya nakula unga na mifano ipo watu ambao wameingia kitika hayo mambo”.

Young Dee alimaliza kwa kusema kama kweli maneno yanayosemwa mtaani yana ukweli basi watu watagundua haraka, “mi ambacho naweza kusema unga hauna siri haufichiki so kama mi nakula unga people they can easily notice haraka sana”

LEO PATAKUWA HAPATOSHI UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR!! NANI ATAMPAKATA MWENZAKE?..

Watani wa jadi nchini Simba na Yanga leo jioni wanashuka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kupambana katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, huku Simba ikiwa na rekodi nzuri ya kuifunga Yanga mabao 5.

Kila upande umekuwa ukitamba kuibuka na ushindi leo

MWANAMKE MWATHIRA WA UKIMWI ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUMNYONYESHA MAZIWA MTOTO WA JIRANI YAKE MAKUSUDI

MWANAMKE   mmoja raia wa Zimbabwe aliyenyonyesha mtoto wa jirani bila ruhusa anakabiliwa na kifungo cha karibu miaka miwili kwa kumwambukiza mtu  HIV kwa  kukusudia kwa  kuwa  yeye  ni  mwathirika.
Annie Mpariwa, 39, alifikishwa mbele ya mahakama ya Gaborone  wiki iliyopita  na kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 24 kuruhusu kipimo cha pili cha HIV kufanyiwa mtoto huyo.
  Matokeo ya kwanza ya mtoto huyo yalionyesha hana virusi ilhali ya mama huyo yalikuwa na virusi. 

Mpariwa alikamatwa wiki jana kwa mashtaka ya usumbufu na iwapo mtoto huyo atapatikana na virusi,  mashtaka hayo yatazidishwa hadi 'kumwambukiza mtu mwingine HIV kimakusudi.’ 

Mama wa mtoto huyo wa miezi 14, Nyasha Mironga, alisema kumwona mwanawe akinyonyeshwa na jirani wake lilikuwa ni jambo lililomshtua sana. 

Kisa hicho kimetokea baada ya kupitishwa kwa sheria mpya ya HIV/Aids inayotoa adhabu kali zaidi kwa wale wanaowaambukiza wengine HIV kimakusudi

NILIINGIA KWENYE MUZIKI KWA KUFUATA MKUMBO: SALMA JABU NISHA

Actress maarufu nchini Salma Jabu(Nisha) amesema kuwa aliingia katika muziki wa Bongofleva kwa kufuata mkumbo baada ya kuwaona waigizaji wenzake wengi wakiingia katika muziki na yeye ndiyo akajitumbukiza na matakeo yake kukaa sana kimya na kupotea katika fani hiyo. Nisha amesema kuwa hatathubutu tena kufuata mkumbo kwenye fani nyingine bali yeye ameamua kujikita zaidi
kwenye fani yake ya filamu. Akizungumza na Gpl star huyo wa filamu za Red-Cross, Matilda, Pusi Na Paku na Tikisa alisema "Niliona waigizaji wanaingia kuimba na mimi nikaingia, nilivamia fani tu ndiyo maana  najuta, nimeamua nikae chonjo kwanza na mambo hayo nijikite zangu kwenye filamu"