MWANAMKE MWATHIRA WA UKIMWI ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUMNYONYESHA MAZIWA MTOTO WA JIRANI YAKE MAKUSUDI

MWANAMKE   mmoja raia wa Zimbabwe aliyenyonyesha mtoto wa jirani bila ruhusa anakabiliwa na kifungo cha karibu miaka miwili kwa kumwambukiza mtu  HIV kwa  kukusudia kwa  kuwa  yeye  ni  mwathirika.
Annie Mpariwa, 39, alifikishwa mbele ya mahakama ya Gaborone  wiki iliyopita  na kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 24 kuruhusu kipimo cha pili cha HIV kufanyiwa mtoto huyo.
  Matokeo ya kwanza ya mtoto huyo yalionyesha hana virusi ilhali ya mama huyo yalikuwa na virusi. 

Mpariwa alikamatwa wiki jana kwa mashtaka ya usumbufu na iwapo mtoto huyo atapatikana na virusi,  mashtaka hayo yatazidishwa hadi 'kumwambukiza mtu mwingine HIV kimakusudi.’ 

Mama wa mtoto huyo wa miezi 14, Nyasha Mironga, alisema kumwona mwanawe akinyonyeshwa na jirani wake lilikuwa ni jambo lililomshtua sana. 

Kisa hicho kimetokea baada ya kupitishwa kwa sheria mpya ya HIV/Aids inayotoa adhabu kali zaidi kwa wale wanaowaambukiza wengine HIV kimakusudi